Jumatatu, 15 Januari 2018

SAIKOLOJIA

Wataalamu wa saikolojia kutoka chuo kikuu cha Penn state Marekani wamegundua katika utafiti wao kuwa zaidi ya 90% ya watoto waliopitia maisha ya kunyanyaswa kupigwa au kudhalilishwa kingono wana balehe haraka ukilinganisha na watoto wanaolelewa kwa upendo.
     Profesor Jamie Noll aliliambia Jarida la Adolescent Health watoto hasa wa kike wanaolelewa kwa kunyanyaswa hasa kupigwa au kubakwa hubalehe kabla ya wakati ukilinanisha na watoto wanaolelewa kwa upendo pia watoto wa aina hii huota matiti mapema ukilinganisha na watoto wa kawaida.
      Akieleza uhusiano ulipo baina ya mtoto kunyanyaswa na kubalehe kabla ya wakati Dr.Noll alisema watoto wanaokuwa katika mazingira kama hayo huzalisha homoni nyingi zinazotokana na msongo wa mawazo hivyo kuharakisha muda wa balehe.

 Wanasaikolojia hao pia walisema mtoto anayenyanyaswa yuko hatarini kupata saratani zaidi kupata saratani ya Ovari na Matiti ukilinganisha na watoto ambao hulelewa kwenye mazingira ya upendo na amani.

Jumapili, 14 Januari 2018

Lishe bora kwa usalama wa mjamzito

Hatari kubwa kwa mjamzito na mtoto  nilishe mbovu
Kwa ajili ya afya ya mama na mtoto ni muhimu sana mwanamke apate chakula bora. Ukosekanaji
wa chakula bora kunaweza kukasababisha mtoto kuzaliwa kabla ya mda wake au na uzito mdogo ambao unaweza ukachangia katika kuzuia ukuaji wa ubongo na mwili.

Kwa mama anaweza akapata anaemia, infection, matatizo katika placenta, matatizo katika labor, c-section(kuzaa kwa upasuaji wakati wa kujifungua), kutokupona kwa haraka, matatizo katika kunyonyesha, toxemia na pre-eclempisa(haya ni magonjwa yanayosababishwa na maini kutoweza kufanya kazi yake vizuri na mwili kujitahidi kutoa protein kutoka sehemu nyingine za mwili kwa sababu hamna protein ya kutosha).

Dalili zake ni pamoja na kuwa na protein kwenye mkojo, blood pressure kuwa juu, kuumwa kwa kichwa, kusikia kizungu zungu, kuzimia, kuvimba kwa viungo n.k

Mama mjamzito anatakiwa apate 100 grams za protein kwa siku.

Ifuatayo ni mlo kamili anaotakiwa apate mama mjamzito kila siku ya ujauzito wake kwa afya bora:

Maziwa na vyakula vya jamii ya maziwa: Glasi nne au zaidi ya maziwa ya aina yoyote pamoja na/au vyakula vyenye jamii ya maziwa kama jibini, mtindi,siagi, ice cream. Maziwa ni muhimu kwa protein, calcium, vitamins na virutubisho vingi. Vitasaidia ukuaji wa mifupa, misuli na nerves. Ni muhimu kwa damu yenye afya, kusaidia usingizi na kusawazisha mdundo wa moyo.

Mayai: Mayai mawili kwa siku husaidia kuupa mwili protein, vitamins minerals na vitamin A ambayo itasaidia kuzuia infections.

Protein: Serving mbili ya samaki, maini , kuku, nyama ya ngombe, mbuzi, kondoo au nguruwe, maharagwe au jibini. Kusaidia ujengaji mifupa, meno, misuli, ubongo na mwili kwa ujumla. Ukosekanaji wa protein ya kutosha kutasababisha kuchoka, uvimbe na kutojisikia kula au appetite ndogo.

Mboga za majani: Spinach, cabbage, collard greends, mchicha, matembele. Mboga hizi ziwe fresh na zile zenye rangi ya kijani iliyokolea(hizi ndio zenye virutubisho vya kutosha). Mboga hizi zitakupa Vitamin A na B, pia virutubisho vitakavyosaidia mwili kuabsorb protein ya kutosha, ukuaji wa mwili, na utengenezaji wa damu. Kutopata mboga za kutosha kunaweza sababisha mama kupata anemia.

Whole Grains: Vipande vinne vya Mkate wa whole grain, mkate wa mahindi, vitaupa mwili vitamin B na carbohydrate kwa ukuaji wa misuli na nerves.

Vyakula vyenye vitamin C: Kipande kimoja au viwili vya machungwa au juisi ya ndimu, machungwa, nyanya. Vitamin C itasaidia uterus kuwa na nguvu ya kutosha ili kufanya kazi vizuri wakati wa labor, pia itasaidia kulinda mwili na infection na kusaidia kuabsorb iron kwenye mwili.

Siagi na mafuta: Serving tatu za maparachichi, siagi, olive oil au flax seed oil.

Matunda yenye rangi ya njano au orange: Huupa mwili vitamin A hii husaidia kulinda kibofu na figo kupata infections.

Maini kama unaypenda ni mazuri kwa protein pia.

Kunywa maji mengi ya kutosha. Maji huchangia kwa asilimia 75 ya uzito wa mtoto wako atakapozaliwa. Usipopata maji ya kutosha utaishiwa na nguvu kwa asilimia 20 na kupata matatizo ya dehydration na kichwa kuuma.

Chumvi ya kutosha kusaidia kuzunguka kwa damu kutoka mwilini kwenda kwenye placenta. Kutopata chumvi ya kutosha kunaweza kusababisha miguu kuuma na uchovu.
Kumbuka kwamba vyakula vyote vinaweza kuwa ni muhimu mwilini lakini huzidiana kulingana na mahitaji na hali ya mtu kwa wakati maalumu.

Mahitaji ya madini na vitamini mwilini wakati wa ujauzito huwa ni makubwa, hususani madini ya kashiamu, chuma na Vitamin B9 (folic acid).

MADINI YA KALISI (Calcium)
Wakati wa ujauzito, madini mengi ya kalisi husafirishwa kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kwa ajili ya kuimarisha mifupa na meno. Katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo, mama huhifadhi madini hayo mwilini mwake. Kiumbe kinapokamilisha umbo lake katika kipindi cha miezi mitatu ya mwisho, hifadhi hiyo huanza kutumiwa na kiumbe hicho, hivyo mahitaji yake kuongezeka.

Katika kipindi hiki, mjamzito anatakiwa kula kwa wingi vyakula vinavyoongeza madini ya kalisi kama vile maziwa na vyakula vitokanavyo na maziwa. Kukiwa na upungufu wa madini hayo, meno ya mama na mifupa huathirika pia.

MADINI YA CHUMA (Iron)
Mahitaji ya madini ya chuma nayo huwa makubwa kwa wajawazito. Madini hayo ni muhimu kwa utengenezaji wa damu ambayo huhitajika kwa wingi na mama pamoja na mtoto.

Madini joto hupatikana kwa kula kwa wingi vyakula kama vile nyama, samaki, mayai, vyakula vilivyopikwa kwa nafaka zisizokobolewa (ugali wa dona, mkate mweusi, n.k) na mboga za majani kama vile spinachi na brokoli. Ili kupata madini hayo ya kutosha kutokana na vyakula hivyo, inashauriwa mjamzito kutumia pia vidonge vya Vitamin C (Vitamin C food supplements).

VITAMIN B9 (Folic Acid)
Vitamini hii ni muhimu sana kwa mjamzito, ni kosa kubwa sana la kiafya kwa mjamzito kuwa na upungufu wa vitamin hii. Vitamin B9 ndiyo inayohusika na ukuzaji na uimarishaji wa mfumo wa fahamu wa kiumbe tumboni.

Aidha, Vitamin hii ndiyo inayotoa kinga ili viungo vya mtoto visiathirike na kuepusha uzaaji wa watoto walemavu au wenye kasoro za viungo kama ‘midomo ya sungura’ na kadhalika.

Vyakula vyenye kiwango kikubwa cha Vitamin B9 ni pamoja na mboga za majani, juisi ya machungwa, mapeasi, vyakula vilivyopikwa kwa ngano na mchele (hasa brown rice) na mayai.

Hata hivyo, kutokana na hali ya vyakula vyetu, mjamzito hawezi kupata kiwango kinachotakiwa cha vitamin hiyo kwa kula vyakula peke yake.

Ili kupata kiwango cha vitamin hiyo kinachotakiwa, mjamzito atatakiwa kutumia pamoja na vidonge vya lishe vya Vitamin B9 ili kuepuka upungufu huo. Inashauriwa kutumia vidonge hivyo miezi michache kabla ya kushika mimba na katika kipindi cha miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito, kipindi ambacho vitamin hiyo huhitajika kwa wingi.

Kwa ujumla, lishe bora ni muhimu kwa mjamzito katika kipindi chote cha ujauzito wake. Matatizo mengi ya kuzaa watoto wenye ulemavu wa aina mbalimbali, hutokana na upungufu wa madini na vitamin muhimu mwilini katika kipindi cha ujauzito.

Jumamosi, 13 Januari 2018

Sababu ya kujifungua kwa operesheni

Kuna sababu mbali mbali zinazosababisha wanawake wa siku hizi kushindwa kufunguka kwa njia ya uzazi na kuwalazimu kupewa madawa kuongeza uchungu au hata kutakiwa kuzaa kwa operesheni/visu/ c-section. Hapa nitajaribu kuchambua kila sababu na ni kwa kivipi hili linachangia.

1. Mazoezi

Wanawake wa zamani walikuwa wakifanya shughuli nyingi sana kama kutembea kwa muda mrefu ili kufika sehemu wanazotaka. Walikuwa wanafanya shughuli nyingi za ndani na nje ambazo wanawake wengi wa siku hizi hawafanyi. Shughuli hizi zilikuwa ni mazoezi tosha, zilizokuwa zikisaidia mwili wa mwanamke kufunguka na kulegea katika kipindi hiki. 

Ila wanawake wa siku hizi mara nyingi wanafanya kazi ofisini, tunaenda kwa magari, unafika ofisini umekaa kwenye kiti, umerudi nyumbani unakaa tena kwenye kochi ukila chakula umekaa kwenye meza ya chakula kwenye kiti, kazi nyingi zimerahisishwa na mashine na hata wasaidizi wa nyumba unaishia kulala tu au kukaa tena kwenye kochi mbele ya tv, computer au simu. 

Siku hizi shughuli nyingi za binadamu zinatumia akili na ubongo zaidi ya mwili. Ndio imerahisisha maisha yetu ya kila siku ila sasa mwili wetu unashindwa kufanya kazi yake vizuri na unakuwa mzembe. 

Ndio maana siku hizi tunashauriwa kutenga muda maalum kufanya mazoezi ili kufidia kuupa mwili mazoezi ya kutosha. Na ni muhimu sana kwa mwanamke mjamzito kufanya mazoezi maalum ili kusaidia kupanua na kuongeza njia ya uzazi. Na sio kufanya mazoezi yoyote yale bali yale muhimu ambayo yatasaidia kuongeza na kupanua njia na misuli maalumu ya uzazi. 


. Lishe na diet


Siku hizi lishe bora haizingatiwi na watu wengi kama zamani. Kutokana na kubadilika kwa maisha ya kila siku na kurahisishwa kwa upikaji na utengenezaji wa chakula mara nyingi hatupati lishe bora.

Watu wengi utakuta wanaenda kazini wanashindwa kuchagua chakula bora wanakula tu chakula kile ambacho kipo mitaani kwa haraka warudi ofisini. Uongo mbaya vyakula ni vitamu lakini si vizuri kwa afya zetu.

Mara nyingi vyakula hivi sio vizuri kwa vile wauzaji wa chakula wanafanya biashara utakuta vyakula hivi vina mafuta mengi na fructose ili waweze kuvitengeneza kwa muda mfupi na kuvifanya viwe na ladha tamu. Vyakula hivi haviko balanced yaani havitoshelezi mlo kamili wenye virutubisho vyote muhimu kwa binadamu hasa hasa kwa mama mjamzito.
*(fructose mbaya ni ile ambayo inatumiwa kama sukari na kuongezwa kwenye vyakula vya viwandani. Fructose ya aina hii sio ya asilia inakuwa imekuwa processed. Siongelei ile ambayo iko naturally kwenye matunda)
Kama mama mjamzito anashindwa kupata lishe bora basi mwili utashindwa kufanya kazi yake vizuri kumtosheleza mama na mtoto. 

Mara nyingi kinachotokea utakuta mama na mtoto wanaongezeka uzito lakini huu sio uzito mzuri unaowafaa. Hivyo mtoto anaweza akawa mkubwa sana na inawia vigumu kwa njia ya uzazi kutosha. 

Mara nyingine mwili wa mama pia unashindwa kufanya kazi ipasavyo kwa vile vyakula vingi vya siku hizi vina kemikali na hormone mbali mbali ambazo si nzuri kwa binadamu na zinauwezo wa kuaffect zoezi zima la kuzaa ikiwa ni pamoja na ufungukaji wa njia ya uzazi. 

Mama mjamzito anatakiwa achukue hatua maalum kupangilia chakula ikiwezekana aandike kama ratiba na ajaribu kufuatilia chakula gani anakula kuona kama anapata mlo kamili. Pia ajaribu kuandaa vyakula vyote mwenyewe na kununua vyakula amabyo ni organic na natural ambavyo havijaongezwa madawa na kemikali viwandani. 

3.Jamii kutokuwa na subira na wamama wajawazito pamoja na uingiliaji wa wauguzi katika shughuli nzima ya kujifungua.


Kuna mara kadhaa ambapo hospitali inaweza kutokadiria vizuri tarehe za kuzaliwa mtoto. Mama, familia, marafiki na hata madaktari wakifuatilia hizi tarehe kama maandiko kutoka kwa Mungu inaweza ikawa ni tatizo kwa mama mjamzito pale tarehe au wiki ya kuzaliwa mtoto itakapofika halafu mama bado hajaingia labor au kuanza kusikia uchungu wa kuzaa . Utakuta familia na marafiki wanaanza kumuuliza mama mbona mtoto bado hajaja hii haimsaidii mama bali  humtia woga na wasiwasi kuwa labda kuna tatizo.

Tunabidi tufikirie kama vile ni tunda, hivi sisi tunafahamu ya kuwa lini tunda ambalo liko kwenye mti litakuwa tayari na kuiva? Ni Mungu pekee ndio anafahamu. Mara nyingi tunasubiri mpaka pale limeiva halafu linadondoka lenyewe. Ukijaribu kulitungua kabla halijaiva unakuta chungu na si tamu tena.Kuna watoto wachache wanaweza kuzaliwa kabla ya miezi tisa kuanzia miezi sita hadi wa tisa. Ila wengi wao kwa kawaida huzaliwa katika miezi minane hadi tisa ya uzazi baada ya hapo unaona kuna uwezekano kabisa watoto wengi kuzaliwa kuanzia mwezi wa tisa hadi wa kumi wa uzazi. Na wengine wachache kwenye mwezi wa kumi hadi wa kumi na moja.

Kwanini makadirio ya siku ya kuzaliwa mtoto huwa mara nyingi si sahihi?

  • Kutofautiana kwa mzunguko wa menstruation cycle au mzunguko wa siku za mwanamke. Wanawake wengine wana mizunguko mrefu na wengine wana mizunguko mifupi. 
  • Ukuaji wa kila mtoto ni tofauti, watoto wengine wanahitaji siku zaidi kuendelea kuwa ndani ya tumbo la mama.
  • Wamama wengine wanapoulizwa lini ilikuwa siku ya mwisho wa hedhi ili kukadiriwa huwa hawana kumbukumbu sahihi.
  • Ndiyo maana tunabidi tuchukulie haya kama makadirio na siyo siku maalumu ambayo mtoto atazaliwa. Mtoto anaweza kuzaliwa siku chache baada au hata wiki kadhaa baada ya siku ya makadirio. Kwa kawaida mtoto anaweza kuzaliwa siku yoyote katika wiki ya 37 hadi wiki ya 43.
  • Hata mashine maalum za ultrasound huwa zinafanya tu makadirio na haiwezi kukupa siku kamili ya kuzaliwa kwa mtoto.
Madaktari wanawezaa kuweka pressure kwa mama kuwa mtoto lazima azaliwe sasa. Na wanaweza kukupa sababu kuwa placenta inaweza kuacha kufanya kazi na mtoto kuzaliwa na madhara au hata kufariki.Lakini kutokana na research iliyofanyika risk ya hii kutokea ni ndogo sana. 

Mara nyingi kuna risk zaidi kutokea kama daktari ataingilia kazi ya mwili na kuulazimisha kuzaa kabla haujawa tayari. Kama mama hana elimu yoyote kuhusiana na uzazi au hata kama ana elimu lakini hana confidence, support, msimamo na dhamira, na basi kukubali tu yale anayoambiwa na watu, ni rahisi sana kukubali kupewa madawa ya kuanzisha uchungu. 

Hizi dawa mara nyingi zitaanzisha uchungu lakini kama mwili hauko tayari basi kutanuka kwa uzazi kutachukua muda na hapo ndio maumivu yatakapozidi kuwa makali na mtoto mara nyingi anakuwa affected na haya madawa basi hapo ndio daktari atabidi ashauri kufanyiwa operesheni. Lakini ukweli ni kwamba hii yote haiko necessary.
Sababu nyingine ni pale ambapo labor imeanza lakini inachukua kipindi kirefu. Mara nyingi watu hawafahamu kuwa labour inaweza kuendelea zaidi ya masaa 24 kutokana na mtu na mtu. 

Kwenye filamu mara nyingi wanaonyesha mtu kashikwa na uchungu maji yamemwagika, kazaa hapo hapo kabla hajafika hospitali. Lakini katika maisha ya kawaida ni nadra sana kutokea. Hasa hasa kwa mtoto wa kwanza. Wanasema kuwa avg ni masaa 12 hadi 17 lakini kuna wanawake ambao wanakuwa kwenye labor siku 3 hadi 4 yaani masaa 72 hadi 96 kuna wale ambao wanabahatika na inakuwa fupi masaa mawili hadi matano hivyo inategemea. 

Mara nyingi wale wenye labour ndefu huwa maumivu yanaanza na kutulia na pia njia inachukua muda kufunguka. Kwa wale wenye labor fupi itachukuwa muda mfupi na maumivu yatakuwa makali sana kwa vile njia itapanuka kwa muda mfupi. 

Ila kwasababu watu wengi siku hizi hatuna subira  na wauguzi wanashughuli nyingi hawawezi kukaa kukusubiria wewe tu mpaka uzae hivyo mara nyingi ikipita baada ya masaa fulani wataanza kukupa ushauri wa kukupa dawa ya kuongeza spidi ya labor hii dawa ndiyo itaongeza spidi lakini ndio maumivu yatazidi na kuwa makali kupita kiasi kwasababu yale maumivu ni ya dawa na sio maumivu asilia hapo ndio mara nyingi mwanamke atashindwa kuvumilia na kukubali operesheni. 

Kwa wale ambao labor itachukua muda mrefu inahitajika stamina ya hali ya juu ikiwa pamoja na mwili kuwa fit kwa mazoezi, lishe bora na maji ya kutosha ili kuendelea kuwa na nguvu kwa kipindi chote hichi. Hapa kama huna stamina ndio hapo kuna uwezekano mkubwa wa kukubali madawa na hatimaye operesheni.

Kama mwanamke anafahamu haya na kajitayarisha vya kutosha unaweza kuendelea na labor nyumbani mpaka ikifikia stage fulani ya labor. 

Tatizo lingine ni position mbali mbali za kuzaa na kumsukuma mtoto. Kuna position ambazo ukikaa wakati wa labor zinasaidia kutanuka kwa njia ya uzazi kwa urahisi zaidi. Lakini mara nyingi hospitalini huwa unaruhusiwa kufanya position moja tu ya kulalia mgongo huku miguu imetanuliwa wakati hii ni position ngumu sana kwa mama kusukuma na njia ya uzazi kutanuka. Pia watu wengi hawafahamu hizi position za kuzaa kwa sababu ya kukosa mafunzo.

Sio kwamba madaktari hawana ujuzi, ila mafunzo yao huegemea zaidi kwa kutumia njia za kisasa kuokoa maisha ya mwanadamu. Pia mara nyingi wana majukumu mengi na kuelemewa na kazi. Hivyo ni responsibility yetu sisi kufahamu mambo gani yanahitaji daktari kuingilia au la. 
Sijui kama hili linaendelea kwa tanzania lakini kwa nchi nyingine ulimwenguni hasa kama marekani mara nyingi hospitali na daktari watalipwa zaidi kama mama atashauriwa kuzaa kwa operesheni au c-section, hivyo imekuwa kama biashara fulani. Inasikitisha lakini ndio ukweli wa maisha.

Ndio maana kipindi cha zamani wanawake walikuwa wanazalishwa na mkunga (midwife) wanawake wazee katika jamii wenye uzoefu wa kutosha, ujuzi na subira katika shughuli nzima ya uzazi. Hawa wakunga walikuwa na ujuzi wa kiasilia ya jinsi ya kupambana na matatizo mbali mbali na hasa kumsaidia mwanamke mjamzito kupanua njia yake kwa njia hizi. Lakini tumepoteza hizi mila na tamaduni mbali mbali.

4. Maumivu kuonekana kama ni kitu kibaya

Nikirudi katika mambo ya mtazamo wa jamii, maumivu ya uzazi yanaangaliwa kama ni maumivu makali kuliko yote kwa mwanamke. Ndio maumivu ni makali lakini jamii haimfundishi mwanamke njia mbali mbali asilia za kukabiliana na maumivu haya. Pia kama mwanamke hana mafunzo, confidence, dhamira na support ya kutosha hataweza kuyastahimili maumivu haya. 

Hivyo pale asikiapo tu maumivu makali na daktari akisema anaweza kumpa kitu kupunguza maumivu wengi wetu hukimbilia kukubali wengine huomba wenyewe hata bila kupewa. 

Kitu ambacho hatufahamu ni kwamba madawa haya mbali na kupunguza maumivu yanauwezo wa kuleta effects nyingine kwa mama mjamzito na mtoto ambazo husababisha daktari kulazimika kufanya operesheni. 

Madhumuni ya maumivu ya uzazi ni kumsukuma mtoto chini na kutanua njia ya uzazi. Hivyo tukiingilia hii kazi kwa kutumia kemikali ndio pale kuzaa kunaweza kuishia kuwa kwa operesheni.

5.Mafunzo, elimu na support pamoja na Mtazamo mbaya kuhusiana na mimba na kuzaa katika jamii

Kwa sababu hamna mafunzo maalumu ya uzazi ya kuaminika kutoka kwa mama zetu au mkunga mwenye ujuzi na mambo ya uzazi na hata jamii kwa ujumla. 

Ninaamini tunafundwa mengi kuhusiana na utunzaji wa nyumba na waume wetu katika ndoa au hata kuwa na boyfriend kutoka katika jamii kwa ujumla. Lakini likija katika jambo la kuzaa na uzazi ni kama vile wazungu wanasema ”taboo”. Ni nadra sana kusikia wanawake wanapeana masomo kuhusu uzazi na ukisikia wanaongelea haya mara nyingi wanapoteshana kwa vile wale wanaowahadithia wenzao pia hawana ujuzi au utaalamu unaotosha. Mara nyingi story zinazoongelewa ni za kutishana tu. 

Ili mwanamke mjamzito aweze kuzaa kwa njia natural anabidi kwanza apate mafunzo ya kutosha kuhusiana na mwili wake kwa kipindi hiki ili afahamu jinsi ya kujitunza na pia ili afahamu kama kuna tatizo au la.  

Pia anabidi apate support ya hali ya juu kutoka kwa jamii inayomzunguka na wale watu karibu kwake ili aweze kuwa na confidence ya kukabiliana na uzazi. Mara nyingi kwasababu wanawake wengi hawajui kitu chochote kuhusiana na kuzaa au labor kwa ujumla tunakuwa kama victims tunasubiri tu siku ifike tuende hospital madaktari na manesi wafanye kila kitu. 

Ila mkiwa na elimu ya kutosha kuna vitu ambavyo munaweza kufanya kurahisisha zoezi zima la kuzaa ikiwa ni pamoja na njia natural za kufungua uzazi, jinsi ya kutambua dalili mbali mbali za labor kuanza, ni vitu gani vitatokea na ni vya kawaida, ni vitu gani ni hatari na jinsi ya kukabiliana na mambo haya.   

Pia kwa sababu ya uoga na kutokufahamu wanawake wengi wanapanga tu kufanya operesheni  kwa vile hawafahamu kuna njia natural za kupambana na mumivu ya labor na madhara ya dawa mbali mbali ambazo zinaweza kutolewa wakati wa kuzaa. 

Pia support katika familia ni kitu muhimu sana kama hamna mtu katika familia yako anafahamu chochote kuhusiana na hili. Basi inamwia vigumu mwanamke kukabiliana na mambo mbali mbali yatakayotokea na kufanya maamuzi ya busara.

Support kutoka kwa familia na elimu au mafunzo pia itamsaidia mwanamke kuweza kuchagua wauguzi wazuri zaidi ambao watakubaliana na maombi yake na kumsikiliza.

Jamii nayo kuzidisha woga kwa mwanamke:

Kila kukicha huwa tunasikia story jinsi mwanamke mwingine alivyopata experience mbaya wakati wa uzazi.  Ukimuuliza mwanamke yoyote yule ambaye hajazaa au hata yule ambaye amezaa lakini hakuwa na experience nzuri kuwa kwanini wanaogopa kuzaa watakuambia wanaogopa mambo yafuatayo.

Maumivu makali ya uzazi na kuogopa labda kitu kibaya kitatokea. 

Wengi wanaogopa vitu kama kukatwa huko chini wakati wa uzazi ili kuongeza njia. 

Wanaogopa kuchanika wakati wa kusukuma mtoto. 

Wanaogopa uke kutanuka na kutorudi katika hali ya kawaida na kuharibu raha au kusikia maumivu wakati wa tendo la ndoa. Wanaogopa mtoto kupatwa na tatizo au kufariki au hata mama kupatwa na tatizo wakati wa kuzaa. 

Wanaogopa kujiachia haja kubwa wakati wa kusukuma mtoto. Wengine wanaogopa kuzaa kwa operesheni.

Kwa kweli kuzaa si kazi lelemama na nasema hivi sio kwa kutisha ila tuichukue kama changamoto ya kwamba tujifunze jinsi ya kukabiliana na siku hiyo muhimu ili mwili uweze kufanya kazi yake kisahihi.

Katika swala hili zima la elimu kwa mwanamke mjamzito ningependa kushauri wanawake wote pale wanapogundua kuwa wana ujauzito au wanataka kupata ujauzito basi washauriane na baba wa mtoto au mtu wa karibu kwako kupata mafunzo maalumu ya uzazi. (birth classes)

Mchukue muda msome mambo kuhusiana na uzazi kwenye tovuti mbali mbali hasa hasa mambo kuhusiana na kuzaa kwa njia ya kawaida. Vitu kama ni mambo gani yatatokea wakati wa kuzaa na jinsi ya kukabiliana nayo.

Kuna website nyingi sana online kutoka kwa wanawake ambao wamezaa kwa njia ya kawaida na wana experience nzuri.(nadhani hapo mbele ninaweza kutoa links za tovuti nzuri kwa hili kama kuna watu wangependa kuzifahamu) Ukisoma story hizi na kuangalia video mbali mbali fupi zinazonyesha story  zao, utapata faraja hata confidence kuwa inawezekana kuzaa kwa kawaida. 

Hii itaondoa woga na wasi wasi ambao ni mojawapo cha chanzo cha matatizo katika kujifungua. Wakati mwingine zoezi zima la kuongezeka kwa njia la uzazi linaweza kusita kama mwili uko stessed, na umejawa na woga au anxiety.

Ijumaa, 12 Januari 2018

SAIKOLOJIA
Tabia za makuzi kwa watoto,Je unafahamu kuwa unapokuwa unaongea ukiwa na mtoto mchanga, anakuwa anakusikia na anakuelewa, au kuandika ujumbe kwenye simu au computer huku anatazama, anakuwa anasoma na kuelewa unachokiandika?

Inakuja kuthibitika atakapokuwa mkubwa, kwa kiasi fulani atafanana matendo kama ya kwako. Kwani alisoma ulichokuwa unaandika akiwa mtoto, akasoma, ufahamu wake ukajua kuwa huo ndio mfumo halisi wa maisha, au alikusikia ukiongea, akatambua kuwa huo ndio msingi wa kuishi kwenye maisha.

THIBITISHA. Mtoto akikua unamwita na kumtukania matukano ya ajabuajabu, ndivyo atakavyokuwa hadi ukubwani mwake, hali kadhalika ukiwa unamtamkia mema tangu utotoni kwa kudhamiria toka moyoni mwako, utamfanya mwanao kuwa ni mfano mwema, popote awapo, hata utu uzima wake. Tubadilishe vizazi vyetu kwa kufanya vitu vyema hasa mbele ya watoto.

SAIKOLOJIA

Kabla ya yote unapopatwa na tatizo hili kwa muda mrefu ni vizuri ukaonana na daktari uweze kupata uchunguzi wa kutosha kubaini nini hasa inaweza kuwa ndiyo sababu hasa ya tatizo kwa upande wako.

Zifuatazo ni dawa mbadala 6 unazoweza kuzitumia ukiwa nyumbani ili kurekebisha tatizo hili

1. Papai

Papai ni moja ya dawa nzuri sana katika kutibu tatizo la kuvurugika kwa hedhi. Ina viinilishe mhimu kama carotene, chuma ( iron), Kalsiamu (calcium) na vitamini A na C ambavyo husaidia kulainisha na kunywea kirahisi kwa kuta za mji wa uzazi.

Siku 2 au 3 kabla ya kuanza kula papai kila siku nusu papai papai zima kutegemea na ukubwa wake au uwezo wako.

Kwa mtu mwelevu sababu ameshagundua papai laweza kumsaidia hivyo basi atalifanya papai kuwa sehemu ya chakula chake kila siku na si mpaka aumwe tu.

2. Mdalasini

Mdalasini unayo sifa ya kuondoa tatizo la damu kuganda sifa inayoweza kusaidia kuondoa tatizo la maumivu wakati wa hedhi.

Mdalasini ni chanzo kizuri cha nyuzinyuzi (fiber), kalsiamu (calcium), chuma (iron) manganizi (manganese).

• Tengeneza chai ya tangawizi kwa kutumia kijiko kidogo cha mdalasini ya unga na maji kikombe kimoja (robo lita), ipua na uache ipowe kidogo, ongeza asali kijiko kikubwa kimoja ndani yake na unywe. Fanya zoezi hili mara 2 mpaka mara tatu siku 2 au 3 kabla ya kuanza siku zako.

• Au changanya kijiko kidogo kimoja cha mdalasini ya unga na kijiko kidogo kimoja cha asali katika glasi moja ya maji ya uvuguvugu na unywe kutwa mara 2 siku za mwanzoni unapoanza au kukaribia kuingia katika siku zako.

3. Tangawizi

Tangawizi ni dawa ya asili yenye maajabu katika kutibu tatizo la mvurugiko wa hedhi. Tangawizi hufanya kazi mhimu kabisa katika kushusha kiwango cha homoni inayosababisha maumivu ijulikanayo kwa kitaalamu kama ‘prostaglandins’.

Tangawizi husaidia pia katika kupigana na uchovu uletwao na mzunguko wa hedhi katika siku zile za mwanzo au siku 2 hivi kabla ya kuanza siku zako na huweza pia kufanya mzunguko usio sawa wa hedhi kuwa sawa

• Tengeneza chai ya tangawizi ukitumia tangawizi mbichi, kunywa kikombe kimoja kutwa mara 3 wakati wa siku zako au siku yoyote tu kama kinga. Kamulia ndimu kidogo ndani yake na utumie asali kupata radha badala ya sukari.

• Unaweza pia kuongeza tangawizi kwenye vyakula na mboga mboga nyingi unazopika kila siku.

4. KOTIMIRI (Parsley):

Tengeneza juisi ya kotimiri, viazi pori (Beet Root), karoti au matango. Tumia asali mbichi ukitengeneza juisi hii. Hii kotimiri inapatikana kirahisi Dar na Zanzibar ni mboga mboga inayotumika zaidi kwenye mahoteli ya kitalii.

Mboga hii inacho kitu mhimu sana kijulikanacho kama ‘Apiol’ amabcho kazi yake kuu ni kurekebisha na kuweka sawa homoni za kike.

Changanya kwa ujazo sawa yaani kama juisi ya kotimiri ni kikombe kimoja basi ya kiazi pori nayo kikombe kimoja kadharika kwa matango.

Juisi hii ni dawa tosha ya maumivu wakati wa siku za hedhi, hurekebisha mzunguko wa hedhi na imethibitika kuwa bora kuliko dawa nyingi za kizungu.

Kunywa glasi moja ya juisi hii kutwa mara 2.

5. MREHANI

Mrehani au Basil kwa Kiingereza ni mmea mwingine mzuri sana katika kuondoa maumivu wakati wa hedhi na kurekebisha mzunguko wa hedhi kwa ujumla.

Mmea huu unatumika sana jikoni kwenye mahotel ya kitalii Dar na Zanzibar. Unao sifa kuu ya kuzuia au kuondoa maumivu mwilini.

• Ongeza kijiko kikubwa kimoja cha majani freshi ya mrehani yaliyokatwakatwa na kisu (chop) kwenye kikombe kimoja cha maji ya moto, funika vizuri na usubiri ipowe. Kunywa yote ikishapoa na ufanye zoezi hili kutwa mara 3 kwa wiki 3 mpaka 4 au mpaka tatizo lako limeisha.

• Au tengeneza juisi ya majani haya. Yatwange kwenye kinu au kwenye blenda ya umee kupata majimaji yake kisha chota vijiko vya chai viwili uweke ndani ya kikombe kimoja cha maji ya moto na unywe yote. Fanya zoezi hili kutwa mara 3.

• Unaweza pia kuongeza majani freshi ya mrehani kwenye vyakula vingi unavyokula kila siku.

6. MAJI YA KUNYWA



Matatizo karibu yote mwilini chanzo chake ni mwili kutokuwa na maji ya kutosha. Maji ni uhai. Unachohitaji hapa ni kutokusubiri kiu. Kiu ni ishara ya mwili iliyochelewa kuhitaji maji.

Matatizo mengi ya kiafya tumeyaona kwa watu wasiopenda kunywa maji ya kutosha kila siku.

Jitahidi hata iweje iwe unaumwa au huumwi chochote unywe maji lita mbili mpaka tatu kila siku iendayo kwa Mungu na utaniletea mrejesho hapa hapa.




Alhamisi, 11 Januari 2018

MTAMBUE MTU ANAE KUDANGANYA BOFYA HAPA

Mwana saikolojia J.J. Newberry mtaalamu wa masuala ya tabia aliwahi kusema kuwa ni kazi rahisi kumtambua mtu muongo endapo utajifunza mbinu za kumfahamu, lakini akaongeza kuwa ni vigumu sana kumnasa muongo kwa njia za kubahatisha. Huu ni ukweli kwamba, wengi huongopewa na wapenzi wao na kujikuta kwenye utata wa kuamini wanachoambiwa na wenza wao ni cha kweli au uongo.
 “Nimechelewa kwenye foleni, nilikwenda kumtazama  mama mgonjwa” Maelezo haya ukiyaangalia unaweza kuamini, lakini pengine unapolinganisha na muda aliofika mpenzi wako nyumbani unabaki kwenye utata, kama kweli alikwenda kumuona bibi yake au alikwenda kufanya usaliti? Kwa kutambua hilo, mada hii inakuja na njia 10 za kumtambua mtu anayeongopa.
 MNASE KUPITIA SHUKU
 Njia namba moja ya kumtambua mtu muongo ni shuku. Wataalamu wanasema kuwa kama mlio wa bunduki utatokea na mtu akakimbia bila hata kutazama ulikotoka ujue mtu huyo ana uongo ndani ya nafsi yake na kinachomkimbiza si mlio bali woga wake.
 Kwa maana hiyo kama ataingia mumeo au mkeo ndani na ghafla akaonesha kushtushwa na uwepo wako jua kuwa ana uongo moyoni au akiacha kufanya jambo fulani kwa kuingia kwako tambua kuwa kuna jambo la uongo ambalo linamuongoza. Muulize vizuri.
 MUULIZE  ASILOTARAJIA
 Swali la kushtukiza lisilotarajiwa linaweza kukusaidia kumtambua mtu muongo anasema Sir Walter Scott kutoka Uingereza ambaye ni mshauri wa masuala ya jamii. Anasema waongo wengi wanapodanganya huwa wametayarisha majibu yao, kupitia maswali wanayotarajia kuulizwa. Kwa mfano akisema, kulikuwa na foleni njiani anakuwa na maeneo ameyaweka tayari. “Yaani kutoka Kigogo pale njia panda magari yalikuwa hayatembei kabisa.”
 Sasa ili umnase muulize jambo ambalo haliko kwenye mpangilio wa uongo wake, kwa mfano hivi magari ya kutoka sehemu fulani yanayopitia hapo Kigogo siku hizi yanakatiza wapi kupisha foleni?” Utashangaa anaanza kutoa macho huku akitafuta jibu wakati inawezekana ulichomuuliza si cha kweli, lakini kwa sababu anadanganya atataka kukupa jibu, ujue huyo ni muongo.
 MBANE KUHUSU MAELEZO YAKE
 Waongo wengi huwa hawana kumbukumbu za ziada, wanapodanganya walikuwa wanakunywa baa fulani husahau kutunza kumbukumbu hizo na kujikuta baadaye wanataja kitu kingine au wakakana kutoa maelezo kama hayo. Hivyo unapokuwa na mtu muongo kariri maneno ya kwanza na kisha umuulize baadaye ukitaka ufafanuzi utashangaa yote yameshayeyuka kichwani kwa muongo na kubaki akikutazama asijue la kufanya.
 MTAZAME MUONEKANO WAKE
 O'Sullivan aliwahi kusema watu waongo huwa na sura tofauti wanaweza kucheka wakati nyuso zao zinalia. Au wakati mwingine kupenda sana kupata msaada wa nguvu za mwili kupitia kuchezea vidole au kushika shika majani.
 Kwa mfano unapokuwa unamtongoza mwanamke ukiona anaacha kukuangalia na kuanza kuchezea vidole au kijiti jua amekukubali hata kama kinywani ataendelea kukataa. Watu waongo nao huficha uongo wao kwa njia hizo. Hivyo unaweza kumtambua muongo kwa kutazama muonekano wake wakati akiongea na wewe.
 MTISHE KWA ADHABU
 Njia nyingine ya kumtambua mtu muongo, ni kumtisha kwa kuchukulia hatua za kustahili na kosa lake. Mapema tu katika mazungumzo yako unaweza kumwambia hivi: “Kwa kuwa umenichosha kwa tabia zako leo lazima niujue ukweli na nitahakikisha unachosema kina ukweli” Si unasema umechelewa kazini, mimi niko tayari kumpigia simu bosi wako kumuuliza” Baada ya kumpa maneno kama hayo ya vitisho anza kumuuliza, utaona anavyokuwa mpole maana anajua akikutajia alikwenda kwa rafiki zake utataka kwenda huko au kumpigia simu hivyo atalazimika kusema ukweli.
 TAMBUA KUPITIA ISHARA ZA MACHO

Paul Ekman mwanasaikolojia kutoka Chuo cha California Medical School cha San Francisco, anasema  mawazo yanayokuwemo ndani ya moyo wa mwanadamu hujulikana kupitia uso wake. Mwenye huzuni moyoni hutambulika usoni hata kama mhusika atakuwa akicheka kama nilivyosema na kadri ukweli wa jambo unavyozidisha msukumo moyoni uso nao hubadilika kulingana na ukweli huo, hata kama mtu atakuwa ameshikilia msimamo wake wa kukataa kukiri ukweli. Msome mtu kwa
kumtazama usoni na usimpe nafasi ya kutazama pembeni.
 ANGALIA MKANGANYIKO
Njia nyingine ya kumtambua mtu muongo ni kumchunguza kuhusu mkanganyiko wa maelezo yake na ishara anazozitoa kupitia kichwa au mikono yake. Mtu muongo unaweza kumuuliza jambo kichwa kikakataa, maelezo yake yakakubali. Hivyo ni vema kufuatilia uhusiano wa maneno, ishara za mwili, sauti yake na vitendo vyake. Ukiona vinapishana tambua kuwa huyo ni muongo.
 KUHUSU HALI YAKE YA KAWAIDA
 Mtu muongo unaweza kumtambua kupitia kawaida yake, ikiwa mpenzi wako ni mtu wa furaha anapokutana nawe lakini ikatokea bila sababu yoyote anapoteza furaha na kutoona umuhimu wako tambua kuwa ana uongo moyoni mwake unamsumbua, ni vema ukamuuliza.
 MAELEZO MENGI
 Wapenzi wenye uongo huwa na maelezo mengi, utakuta kitu kidogo tu cha kujibu ndiyo au hapana yeye anatoa maelezo mengi yasiyokuwa na msingi. Ukiona hivyo tambua kuwa mpenzi wako ana tabia ya uongo na kwamba anarefusha maelezo ili kuujenga uongo wake uonekane ni kitu cha kweli.
 USIPUUZE UKWELI
 Pamoja na mambo yote tuliyojifunza kuhusu waongo, si vema kuyapuuza yote kwa sababu tu umebaini kuwa mtu fulani ni muongo, lazima ya ukweli yapewe nafasi yake. Kwa mfano muongo anapoeleza jambo la kweli muunge mkono, ili kumfanya mwenyewe atofautishe ukweli na uongo anaopika. Ukikataa yote atakuona wewe ndiyo muongo kwa vile utakuwa umekataa mambo ya ukweli aliyokuambia.
SABABU 6 ZA KUKOSA / KUCHELEWA KUPATA HEDHI
Kwa mwanamke kuchelewa kupata hedhi huwa hakushitui endapo mwanamke atakua anajua ni nini tatizo au sababu iliyopelekea yeye kukosa hedhi. Na majibu ya kuchelewa kwa hedhi hupatikana pindi hedhi hiyo inapochelewa. Mfano kama ulikua unategemea kupata mimba, ikichelewa inakua ni dalili ya kwanza ya wewe kuanza kufikiria jambo ulilolitaka ninaelekea kutimia na hata ukatabasamu na kuwaza hatua nyingine ya kujipima nyumbani au kuenda hospitali. Na kama hukuwa umetarajia ndio hivyo tena mawazo ya kila aina yatakuja kichwa kutaka kujua kwanini hedhi yako imechelewa na pengine usipate majibu kabisa.
Hapa nimekuwekea sababu 6 zinazoweza kusababisha hedhi ya mwanamke kuchelewa, na nimefanya hivi kwa kutambua kwamba wanawake wengi hufikiria sababu moja tu endapo hedhi yao itakua imechelewa.
1 . Mimba
Hii ndio sababu ya kwanza kuja kichwani endapo siku za hedhi za mwanamke zitakua zimechelewa. Na inawezekana ukawa sahihi!! Na hii hutokea hata kama mwanamke alishapata dalili zote za kwamba siku zake za hedhi ziko njiani, ila siku uliyotarajiwa ishuke inakua haishuki. Mara nyingi huwa tunashindwa kabisa kujizuia kufikiria neno MIMBA!! Hata kama mtu anafahamu kabisa hakucheza rafu mwezi huo. Kwa ushauri tu ili usipatwe na msongo wa mawazo zaidi tafuta kipimo binafsi au kama ni ngumu pitia hospitali upate vipimo.
2 . Msongo wa mawazo.
Msongo wa mawazo huleta madhara katika mwili wa binadamu mara nyingi sana, mfano kuumwa kichwa, kuongezeka uzito, kuota vipele na hata vidonda vya tumbo, na kama nilivyosema awali , kama tayari umeshajua kwamba hedhi imechelewa msongo wa mawazo unaoupata kwa kufikiri sababu ni mimba ikiwa haukuwa umeitarajia unaweza kufanya mwili usiwe katika hali yake ya kawaida tena na hivyo kuendelea kusababisha kuchelewa kwa siku za hedhi zaidi na zaidi. Kwenye mwili wa mwanadamu kuna homoni mbili ziitwazo ‘adrenaline na cortisol’. Hizi hufanya maamuzi kwenye mwili ya kipi kinaumuhimu zaidi ya kingine mpaka msongo wa mawazo utakapokuisha. Mara nyingi homini hizi huamua kuanza kazi katika vitu kama msukumo wa damu na gesi mapafuni, huku kazi nyingine kama mmeng’enyo wa chakula na mfumo wa kizazi kufuatia baadae  na hivyo hata hedhi itachelewa kushuka kama tatizo ndio hilo.
3 . Ugonjwa
Ugonjwa wowote unaweza sababisha hedhi kuchelewa kwa hedhi, hata kama ni mafua au malaria. Ugonjwa uliona kwa wakati huo utakua ni kipaumbele cha kila homini mwilini mwako kuundoa kama nilivyoelezea hapo juu kwa homoni zako kutoa kipaumbele kwa mifumo muhimu zaidi ya kizazi kwa wakati huo.
4 . Kubadilisha mazingira.
Kubadili mazingira kwa hapa naamaani chochote kile ulichokua unafanya zamani, ukakicha ghafla mfano ulikua unaishi sehemu ya baridi ukahamia yenye joto na kinyume chake, au kusafiri muda mrefu, kama ulikua unafanya kazi usiku tu ukaanza kufanya kazi mchana mara nyingi hii husababisha kukosa au kuchelewa kwa hedhi. Usihofu endapo unajua ulifanya nini mwezi huo.
5 . Kunyonyesha
Kama unanyonyesha hautaona hedhi kwa muda mrefu, japo hutofautiana kutokana na maumbile ya kila mwanamke kwa sababu prolactin ( Homoni inayowezesha uzalishaji wa maziwa ya mama ) huharibu kupevuka kwa yai (ovulation) . Wamama wengi hua hawapati hedhi kwa miezi pale wanapokua wananyonyesha . Lakini kumbuka , kukosa hedhi haimaanishi kwamba hauwezi kushika mimba , kwa sababu ovulation hutokea kabla haujapata hedhi yako, inawezekana yai likapevuka na baadae ukapata mimba kabla hata haujapata hedhi . Kwahiyo ukiwa unanyonyesha hakikisha unatumia kinga.
Madawa
Ukweli ni kwamba kuna dawa maarufu za kusababisha kuchelewa kupata hedhi. Hizi ni kwa matumizi ya uzazi wa mpango. Dawa hizi huzuia ovulation kwahiyo kama hakuna ovulation basi hakuna hedhi. Na hizi unaweza fahamu kama unazitumia kwa hiyo hedhi ikichelewa unakuwa huna wasiwasi, na kama hufahamu basi endapo utaongea na daktari anayekupangia dawa za uzazi wa mpango kumbuka kumuuliza madhara yanayotokana na matumizi ya dawa hizo (side effects) atakazokupa.