Ijumaa, 12 Januari 2018


Kabla ya yote unapopatwa na tatizo hili kwa muda mrefu ni vizuri ukaonana na daktari uweze kupata uchunguzi wa kutosha kubaini nini hasa inaweza kuwa ndiyo sababu hasa ya tatizo kwa upande wako.

Zifuatazo ni dawa mbadala 6 unazoweza kuzitumia ukiwa nyumbani ili kurekebisha tatizo hili

1. Papai

Papai ni moja ya dawa nzuri sana katika kutibu tatizo la kuvurugika kwa hedhi. Ina viinilishe mhimu kama carotene, chuma ( iron), Kalsiamu (calcium) na vitamini A na C ambavyo husaidia kulainisha na kunywea kirahisi kwa kuta za mji wa uzazi.

Siku 2 au 3 kabla ya kuanza kula papai kila siku nusu papai papai zima kutegemea na ukubwa wake au uwezo wako.

Kwa mtu mwelevu sababu ameshagundua papai laweza kumsaidia hivyo basi atalifanya papai kuwa sehemu ya chakula chake kila siku na si mpaka aumwe tu.

2. Mdalasini

Mdalasini unayo sifa ya kuondoa tatizo la damu kuganda sifa inayoweza kusaidia kuondoa tatizo la maumivu wakati wa hedhi.

Mdalasini ni chanzo kizuri cha nyuzinyuzi (fiber), kalsiamu (calcium), chuma (iron) manganizi (manganese).

• Tengeneza chai ya tangawizi kwa kutumia kijiko kidogo cha mdalasini ya unga na maji kikombe kimoja (robo lita), ipua na uache ipowe kidogo, ongeza asali kijiko kikubwa kimoja ndani yake na unywe. Fanya zoezi hili mara 2 mpaka mara tatu siku 2 au 3 kabla ya kuanza siku zako.

• Au changanya kijiko kidogo kimoja cha mdalasini ya unga na kijiko kidogo kimoja cha asali katika glasi moja ya maji ya uvuguvugu na unywe kutwa mara 2 siku za mwanzoni unapoanza au kukaribia kuingia katika siku zako.

3. Tangawizi

Tangawizi ni dawa ya asili yenye maajabu katika kutibu tatizo la mvurugiko wa hedhi. Tangawizi hufanya kazi mhimu kabisa katika kushusha kiwango cha homoni inayosababisha maumivu ijulikanayo kwa kitaalamu kama ‘prostaglandins’.

Tangawizi husaidia pia katika kupigana na uchovu uletwao na mzunguko wa hedhi katika siku zile za mwanzo au siku 2 hivi kabla ya kuanza siku zako na huweza pia kufanya mzunguko usio sawa wa hedhi kuwa sawa

• Tengeneza chai ya tangawizi ukitumia tangawizi mbichi, kunywa kikombe kimoja kutwa mara 3 wakati wa siku zako au siku yoyote tu kama kinga. Kamulia ndimu kidogo ndani yake na utumie asali kupata radha badala ya sukari.

• Unaweza pia kuongeza tangawizi kwenye vyakula na mboga mboga nyingi unazopika kila siku.

4. KOTIMIRI (Parsley):

Tengeneza juisi ya kotimiri, viazi pori (Beet Root), karoti au matango. Tumia asali mbichi ukitengeneza juisi hii. Hii kotimiri inapatikana kirahisi Dar na Zanzibar ni mboga mboga inayotumika zaidi kwenye mahoteli ya kitalii.

Mboga hii inacho kitu mhimu sana kijulikanacho kama ‘Apiol’ amabcho kazi yake kuu ni kurekebisha na kuweka sawa homoni za kike.

Changanya kwa ujazo sawa yaani kama juisi ya kotimiri ni kikombe kimoja basi ya kiazi pori nayo kikombe kimoja kadharika kwa matango.

Juisi hii ni dawa tosha ya maumivu wakati wa siku za hedhi, hurekebisha mzunguko wa hedhi na imethibitika kuwa bora kuliko dawa nyingi za kizungu.

Kunywa glasi moja ya juisi hii kutwa mara 2.

5. MREHANI

Mrehani au Basil kwa Kiingereza ni mmea mwingine mzuri sana katika kuondoa maumivu wakati wa hedhi na kurekebisha mzunguko wa hedhi kwa ujumla.

Mmea huu unatumika sana jikoni kwenye mahotel ya kitalii Dar na Zanzibar. Unao sifa kuu ya kuzuia au kuondoa maumivu mwilini.

• Ongeza kijiko kikubwa kimoja cha majani freshi ya mrehani yaliyokatwakatwa na kisu (chop) kwenye kikombe kimoja cha maji ya moto, funika vizuri na usubiri ipowe. Kunywa yote ikishapoa na ufanye zoezi hili kutwa mara 3 kwa wiki 3 mpaka 4 au mpaka tatizo lako limeisha.

• Au tengeneza juisi ya majani haya. Yatwange kwenye kinu au kwenye blenda ya umee kupata majimaji yake kisha chota vijiko vya chai viwili uweke ndani ya kikombe kimoja cha maji ya moto na unywe yote. Fanya zoezi hili kutwa mara 3.

• Unaweza pia kuongeza majani freshi ya mrehani kwenye vyakula vingi unavyokula kila siku.

6. MAJI YA KUNYWA



Matatizo karibu yote mwilini chanzo chake ni mwili kutokuwa na maji ya kutosha. Maji ni uhai. Unachohitaji hapa ni kutokusubiri kiu. Kiu ni ishara ya mwili iliyochelewa kuhitaji maji.

Matatizo mengi ya kiafya tumeyaona kwa watu wasiopenda kunywa maji ya kutosha kila siku.

Jitahidi hata iweje iwe unaumwa au huumwi chochote unywe maji lita mbili mpaka tatu kila siku iendayo kwa Mungu na utaniletea mrejesho hapa hapa.




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Comment yako ni muhimu sana