Ijumaa, 29 Desemba 2017

MATATIZO YA KUKOSA HEDHI KWA WANAWAKE
Wanawake wengi huwa na vipindi vya hedhi kuanzia 11 mpaka 13 kwa mwaka. Hii hutofautiana kwa wanawake. Unaweza kuwa na vipindi zaidi ya hivi au vichache. Kukosa hedhi au kubadilika kwa vipindi vya hedhi itatazamwa kutokana na kile ambacho ni kawaida kwako. Mfano ikiwa unakuja kwenye hedhi tarehe 11-13 kila mwezi, hiyo ndiyo kawaida yako. Mwingine anaweza kuwa anakuja kwenye hedhi tarehe 20-23 kila mwezi , na hiyo ndiyo kawaida yake. Hivyo kawaida  yako inaweza ikawa si kawaida kwa mwanamke mwingine. Ni vyema kutazama siku zako na siyo za mwingine, kuangalia kama una tatizo ama la.
Vipindi vya hedhi huwa vinatofautiana sana hasa  kuelekea miaka ya kukoma hedhi. Wanawake wengi hutambua kwamba wanaelekea karibu na kukoma hedhi  pale vipindi vyao vya hedhi huanza kubadilikabadilika na kutokuwa vya kawaida. Kukoma hedhi hutokea pale unapokuwa na  kipindi cha mwaka mzima (miezi 12) bila kupata hedhi au kwa maneno mengine  miezi 12 tokea umepata hedhi yako ya mwisho.

                                       
Mara nyingi ujauzito ni sababu ya kukosa hedhi. Kama unadhani wewe ni mjamzito tafadhali anza kuishi kama mwanamke mjamzito mpaka pale ukapogundua ya kwamba kweli wewe ni mjamzito ama la. Tumia vipimo vya ujazito vinavyopatika kwenye maduka ya dawa kujipima. Ni rahisi kutumia. Unaweza kusoma maelekezo au kuelekezwa na muuzaji.

SABABU ZA KUKOSA HEDHI AU KUWA NA HEDHI ISIYO YA KAWAIDA

Nimesema sababu ya kwanza kabisa ya kukosa hedhi ni ujauzito. Kama umekosa hedhi na huna kabisa ujauzito, vipo visababishi vingine kama ifuatayo:
  Kuongezeka sana au kupungua sana  uzito wa mwili. Ingawa mara nyingi kupungua uzito ndilo tatizo la mara kwa mara kumfanya mwanamke kukosa hedhi au kuwa na hedhi isiyo ya kawaida lakini pia kuongezeka uzito kunaweza kusababisha matatizo ya hedhi.
 Matatizo ya ulaji mfano kukosa hamu ya kula au matatizo yajulikanayo kwa kitaalam kama  bulimia na  anorexia nervosa.  ‘Bulimia’ ni tatizo ambalo mtu hula sana lakini mara tu baada kula hutapika chakula chote na kufanya mtu huyo kukonda sana na ‘Anorexia nervosa’ ni tatizo ambalo mtu hukosa hamu ya chakula na kumfanya ale chakula kidogo kisichokidhi mahitaji ya mwili .  Hii inampelekea kupoteza uzito
    Kufanya mazoezi ya viungo sana
    Msongo wa mawazo
 Kuumwa
Safari
Madawa kama dawa za uzazi wa mpango. Hizi zinaweza kukufanya ukawa na hedhi nyepesi, isiyo ya mara kwa mara au  kuwa na hedhi mara kwa mara au kuruka vipindi vya hedhi au kukosa hedhi kabisa
   Matatizo ya homoni. Matatizo ya homoni yanaweza kubadili kiwango cha homoni ambacho mwili huhitaji kwa ajili hedhi
   Matumizi mabaya ya madawa
  Matatizo kwenye viungo vya kiunoni kama uvimbe kwenye mji wa mayai ( Polycystic Ovary syndrome, kuziba kwa kiwambo cha uke ( imperforate hymeni) na uvimbe wa kovu kwenye kuta mfuko wa uzazi (  Asherman’s syndrome)
 Kunyonyesha. Wanawake wengi hawezi kurudi kwenye siku zao za kawaida mpaka wanapoacha kunyonyesha

Jumatano, 27 Desemba 2017

TAMBUA DALILI 6 ZA MIMBA KUHARIBIKA
kuna sababu nyingi sana zinazoweza kuharibu mimba ya mama ikiwemo ugonjwa wa malaria, kaswende, kazi nyingi, magonjwa ya zinaa, u.t.i dawa fulani fulani mfano albendazole, misoprostol, metronidazole na kadhalika. lkiujumla sababu nyingi ambazo zinasababisha mimba kutoka huweza kuzuilika kwa kwenda kliniki mapema yaani pale tu unapohisi una mimba hata kama ni wiki mbili na kufuata ushauri wa wataalamu. sasa kuna wanawake wengi mimba zo huharibika na wao hushindwa kugundua mapema na matokeo yake anakaa na mtoto mfu hata miezi kadhaa bila kujua hivyo leo ntaongelea dalili za kuharibika kwa mimba kama ifuatavyo.

1. kutokwa na damu nyingi sehemu za siri; hii ni dalili kwamba mimba imeanza kuachia na mlango wa uzazi umeanza akufunguka sasa ukienda hospitali utakuta majibu mawili kwamba mtoto ameshafia tumboni au bado hajafa. lakini kama imeshatoka damu nyingi mtoto huyu atakufa tu.

2. mtoto kuacha kucheza tumboni; kwa kawaida mtoto huanza kucheza wiki ya 18 mpaka 20 kwa wanawake ambao hawajawahi kubeba mimba na wiki ya 16 mpaka 20 kwa wanawake ambao wamehsawahi kuzaa sasa ikitokea mtoto ameshawahi kucheza na sasa hachezi tena au muda huo umepitiliza na bado kimya kuna uwezekano mkubwa ameshafariki.

3. kupotea kwa dalili za ujauzito; mara nyingi mtu akipata ujauzito anakua na dalili nyingi kama kichefuchefu, kukosa hamu ya kula, kutapika sana na kubadilika sana tabia sasa zile dalili zote za mimba zikisimama ghafla basi ujue mimba imeharibika.

4. kuacha kuongezeka kwa mimba; tunategemea mimba kuendelea kua kubwa kulingana na umri unavyozidi kwenda mbele sasa kama mimba mara ya mwisho ilikua na miezi mitatu na leo ina miezi sita au mitano lakini iko haijabadilika ukubwa ujue mimba imeharibika.

5. maumivu makali ya tumbo; maumivu makali ya tumbo hasa kwa mimba kubwa sana au mimba ndogo sana kuna uwezekano mkubwa kondo imeanza kujiondoa kwenye kizazi kwa mimba kubwa au mimba ndogo imeshindwa kuendelea kukua. hii inaweza kua dalili kwamba mimba imeharibika.

6. kutoka kwa vipande vya nyama sehemu za siri; vipande vya nyama huashiria kwamba kuna mtoto anakua ameharibika tayari tumboni na mama kama huyu anatakiwa asafishwe kuondoa masalio yaliyobaki ili mama asiweze kupata madhara zaidi.

mwisho; kama nilivyosema mwanzoni mimba nyingi zinazoharibika hasa kwa nchi zetu za kiafrika hua kuna uzembe wa watu kutaka kujitibu wenyewe, kutokwenda kliniki mapema na kutofuata ushauri wa kitaalamu. Hakikisha unakwenda kliniki katika kipindi chote cha uja uzito wako.

Jumanne, 26 Desemba 2017

MATATIZO KATIKA MATITI, CHANZO NA DALILI ...SOMA HAPA
Matatizo ya matiti huwasumbua wanawake wengi na hata wanaume. Matatizo haya yapo ya aina nyingi, mfano uvimbe wa matiti, maumivu ya matiti au matiti kutoa maziwa au majimaji au damu. Tatizo hili hutokea katika umri wote kuanzia pale mwanamke anapovunja ungo hadi anapofikia ukomo wa hedhi.
Matatizo ya matiti katika umri mkubwa kuanzia miaka 35 mara nyingi huambatana na saratani ya matiti. Jinsi tatizo linavyotokea Uvimbe wa matiti upo wa aina mbili. Kwanza ni vivimbe vidogo katika matiti na pili ni uvimbe mmoja mkubwa.
Vivimbe vidogo au mkubwa vinaweza kuwa katika titi moja au yote mawili. Uvimbe huu unaweza kuwa na maumivu au usiwe na maumivu na huwa unazunguka kama utaupapasa, endapo uvimbe utakuwa mgumu na hautembei kuna uwezekano mkubwa wa uwepo wa saratani.
Maumivu ya matiti hutokana na uvimbe kuwa mkubwa, kuvimba mishipa ya damu (Fibrocystic Breast Disease) na maambukizi ya matiti. Maambukizi na matatizo ya mishipa ya damu huwatokea zaidi wanawake wanaonyonyesha ambapo matiti huvimba na huwa na maumivu makali.
Tatizo la matiti kutoa maziwa au maji maji huwatokea zaidi wanawake ambao wamekatisha kunyonyesha, mfano mtoto amefariki au mimba imeharibika. Matiti yana maumbile tofauti kutokana na mtu na mtu, yanaweza kuwa makubwa au madogo, au makubwa wakati wa ujauzito au baada ya kujifungua.
Dalili za matatizo Matatizo ya matiti huonyesha dalili tofauti tofauti kama tulivyoona hapo awali. Dalili hizi zinaweza kujitokeza kwa pamoja au mbili kwa pamoja au moja peke yake. Mfano mtu anaweza kuwa na maumivu na uvimbe au uvimbe na matiti kutoa maziwa.
Pia unaweza kuwa na dalili mojawapo ya hizo nilizoelezea, mfano maziwa kutoka pekee. Matatizo ya matiti huwa na uhusiano mkubwa na masuala ya uzazi, mfano mwanamke unaweza kuhisi matiti yanauma na yamejaa kipindi cha upevushaji mayai au unapokuwa mjamzito,
pia endapo matiti yatakuwa yanatoa maziwa na huna mimba wala historia ya ujauzito, basi ni matatizo ya mfumo wa homoni na uwezekano wa kushika mimba hupotea au haupo. Ni vema endapo una tatizo la matiti kutoa maziwa na unatafuta ujauzito hupati uwaone madaktari wa akina mama kwa uchunguzi wa kina.
Saratani ya matiti Tatizo hili huanza taratibu kama kivimbe kwenye titi moja au yote mawili. Uvimbe huu huendelea kukua taratibu na huwa sehemu moja ya titi. Katika hatua za awali, uvimbe hutembea yaani ukibonyeza unasogea sehemu nyingine na hauna maumivu.
Baada ya kuendelea kukua, uvimbe huwa mgumu kama ubao na hutanuka zaidi na kusababisha ngozi ya juu ya uvimbe huo kuwa na matundu au kama ganda la chungwa, tezi huvimba kwapani na wakati mwingine chuchu huanza kutoa damu.
Uchunguzi Matatizo ya matiti hufanyika katika vituo vya afya ambapo mgonjwa huchunguzwa kufuatana na jinsi tatizo linavyojitokeza. Vipimo vya damu,Ultrasound, X-ray na vingine vitafanyika kadiri daktari atakavyoona inafaa.
Matibabu na ushauri Tiba hutegemea na jinsi vipimo vinavyoonyesha. Mgonjwa atatibiwa kadiri daktari atakavyomchunguza. Dawa za homoni na ufuatiliaji katika mfumo wa uzazi pia utafanyika. Wahi hospitali kwa uchunguzi na tiba. 


Jumamosi, 23 Desemba 2017

tiba ya muwasho Sehemu za siri


Kuwashwa sehemu za siri kunaweza kuwa dalili ya maradhi fulani kujumuisha maradhi ya uke kwa wanawake au muwasho na kuvimba kwa sehemu za siri za wanaume (jock itch). Bila kujali jinsia muwasho unaweza kusababishwa na ugonjwa wa ngozi, magonjwa ya zinaa au mzio (allery).

Kuwashwa makalioni hutokea pale ngozi inayozunguka njia ya haja kubwa inapokereketa ikiambatana na hamu ya kutaka kupakuna. Muwasho huongezeka pale unapokaa na kukiwa na unyevunyevu. Sababu kuu za kuwashwa matakoni ni kutojisafisha vizuri, kula vyakula vyenye viungo vingi sana, kuhara, vidonda kwenye njia ya haja kubwa, maambukizi ya fangasi, bawasiri(hemorrhoids), minyoo na kadhalika.

Mara nyingi muwasho sehemu za siri unaosababishwa na kitu huisha wenyewe kitu hicho kikiondolewa. Vitu vingine vinavyosababisha muwasho huhitaji matibabu ya hali ya juu zaidi, ikiwa unawashwa kwa muda mrefu ni vyema kuzungumza na daktari.

Nini husababisha Muwasho Sehemu za Siri za Mwanaume?

Kuwashwa uume au sehemu zingine za siri za mwanaume husababishwa na sababu zilezile zinazosababisha muwasho sehemu zingine za mwili. Maambukizi hasa ya magonjwa ya zinaa ndio chanzo kikuu cha kuwashwa uume. Sababu zingine ni maradhi ya fangasi, ugonjwa wa upele (scabies), kuwepo kwa chawa, mzio, maambukizi ya bakteria n.k

Nini husababisha Muwasho Sehemu za Siri za Mwanamke?

(1) Maambukizi ya Fangasi Ukeni (Vaginal Yeast Infection)
Ni moja ya tatizo kwa wanawake linalosababishwa na fangasi waitwao Candida. Dalili kuu ni uwashwa ukeni, kuvimba na kutoa uchafu mweupe kama maziwa ukeni.

(2) Ugonjwa wa kuvimba uke (Vulvovaginitis)
Ni ugonjwa unaoathiri kwa kuvimbisha sehemu za nje za uke na uke wenyewe. Dalili kuu ni kuwashwa ukeni, mkojo kuuma na kukereketa wakati wa kukojoa na kutokwa na uchafu ukeni.

(3) Kuvimba Uke baada ya hedhi kukoma (Postmenopausal Atrophic Vaginitis)
Ni ugonjwa wa kuvimba kwa uke baada ya hedhi kukoma. Hali hii huongeza maambukizi ukeni na huweza kusababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa.

(4) Maambukizi ya Trikomonasi (Trichomonas Infection)
Ni ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na kimelea aitwaye Trichomonas vaginalis. Dalili kuu ni muwasho katika uke au uume na kutokwa na uchafu ukeni.

(5) Ugonjwa wa Minyoo (Pinworm Infection)
Ni maambukizi ya minyoo wadogo sana wenye umbo la pini wanaoweza kuambukiza utumbo na kusambaa maeneo mbalimbali. Ugonjwa huu huwatokea sana watoto wa kati ya miaka 5 na 10.

(6) Inflamesheni ya Urethra (Urethritis)
Ni maambukizi kwenye urethra (ujia wa kutolea mkojo nje) yanasababisha kuvimba kwa urethra. Dalili kuu ni mkojo kuchoma, maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kutokwa uchafu.

(7) Genital Warts
Ni vivimbe vidogo vinavyotokea juu ya ngozi sehemu za siri. Ugonjwa unaoenezwa kwa njia ya kujamiana na unasababishwa na virusi viitavyo Human papillomavirus (HPV). Vivimbe vinaweza sababisha muwasho na maumivu.

(8) Saratani ya sehemu ya nje ya Uke (Vulvar Cancer)
Ni saratani ya sehemu ya nje ya uke inayoambatana na kuwashwa sehemu ya nje ya uke.

(9) Ugonjwa wa Wasiwasi (Generalized Anxiety Disorder)
Ni ugonjwa ambao unaotokana na hofu ya matukio fulani. Wakati mwingine husababisha kujikuna sehemu mbalimbali hata sehemu za siri.

(10) Ugonjwa wa Sjogren (Sjogren's Syndrome)
Ni ugonjwa katika mfumo wa kinga ya mwili unaoathiri tezi zinazosaidia mwili kutengeneza unyevu nyevu kwenye macho na mdomo. Ugonjwa huu huathiri wanawake zaidi kuliko wanaume.

(11) Kisukari
Ni ugonjwa sugu wa kimetaboliki unaosababishwa na kasoro katika utengenezaji wa Insulin au utendaji kazi wake. Kisukari kilichokomaa kinaweza sababisha maumivu ya tumbo, kichefuchefu, kizunguzungu na kuwashwa sehemu za siri.

Wanaume wanapaswa kufuata hatua zifuatazo ili kusaidia kuepuka kuwashwa sehemu za siri :-
– Kuosha vizuri uume, na kwa wale ambao hawajatahiriwa wanapaswa kuosha kwa umakini zaidi hadi sehemu za ndani za govi.
– Ziwekesehemu zako za siri kutia ndani makalio katika hali ya usafi na ukavu, kwa maana unyevunyevu unaweza sababisha maambukizi. Matumizi ya poda ya Cornstarch yanaruhusiwa hasa kipindi cha joto kali.
– Vaa nguo isiyobana sana, iliyotengenezwa kwa vitu asilia kama pamba. Badili nguo ya ndani (chupi) angalau kila siku.
– Vaa kondomu kila unapofanya ngono na mwanamke usiyejua hali yake kiafya kiujumla.

Wanawake wanapaswa kufuata hatua zifuatazo ili kusaidia kuepuka kuwashwa sehemu za siri:-
– Baada ya kukojoa au kujisaidia, osha sehemu zako za siri kuanzia mbele(ukeni) kwenda nyuma(matakoni) ili kuzuia bakteria kutoka njia ya haja kubwani kuingia ukeni.

Ijumaa, 22 Desemba 2017

Uongezekaji wa uzito kwa mama Mjamzito
Wanawake wengi huwa wanaogopa kuongezeka uzito sana wakati wa ujauzito kwa sababu ya kupoteza mvuto wao baada ya kuzaa. Kitu ambacho inabidi ukumbuke ni kwamba ukila chakula chenye afya kwa mama mjamzito basi uzito wote utakaoupata kwa wakati huu ni ule ambao mwili wako unauhitaji.

Katika kipindi hichi mwili hufanya kazi kubwa sana katika kutengeneza viungo vya mtoto na pia katika kuujenga mwili wa mama ili uweze kusupport na kumtunza mtoto kwa kipindi kizima cha ujauzito.

Wamama wengi husikia njaa sana wanapokuwa wajawazito na huwa na hamu kubwa ya kula hii ni njia ya mwili kumkumbusha mama kutosheleza mwili kwa ajili ya kipindi hiki maalum. Pamoja na hayo usichukulie hii kama sababu ya kula chakula chochote kile. Mama anabidi apate virutubisho vizuri vinavyotakiwa kwa afya yake na mtoto.

Kula chakula ambacho kina diet na balanced especially kwamama mjamzito ambacho kina protein ya hali ya juu. Usile vyakula vyenye mafuta mengi, sukari au vyakula vya junk food.

Kitu muhimu kwa mama mjamzito ni kuhakikisha hali vyakula vilivyotengenezwa viwandani yaani processed food na junk food, pia vyakula ambavyo haviko natural kwani hivi vinasababisha unene bila kuupa mwili au mtoto virutubisho vya kutosha.

Hivyo mama anahitaji ahakikishe kuwa anakula vyakula natural vilivopikwa nyumbani vyenye protein ya kutosha. Kumbuka ubongo wa mtoto na wa mama umetengenezwa na 75% ya mafuta ya cholesterol. Na ni muhimu sana mama kutosheleza mahitaji yake ya cholesterol kutoka kwenye vyakula vyenye protein ya juu kama vile maziwa. Ndio maana maziwa ni muhimu sana kwa mtoto anayekua ili kuutengeneza ubongo wake.

Je, unapopima uzito huo uzito unaongezeka mwilini huenda wapi? Kumbuka sio uzito wote unaoongezeka wakati wa ujauzito ni uzito wa kunenepa bali:

7.5 – 8 pound ni uzito wa mtoto
2 pound ni za amniotic fluid( yale maji ambayo yanamlinda mtoto ndani ya uzazi)
1.5 – 2pound ni placenta( mfuko wa uzazi)
1.5 -2pound zitaenda kwenda kwenye maziwa kutayarisha utengenezaji wa chakula cha mtoto atakapozaliwa
3lb ni damu ambayo itaongezeka mwilini kuhakikisha unadamu ya kutosha
2 – 2lb misuli ya uzazi
4 pound maji
8 pound ni mafuta ya akiba kutosheleza mwili na kukupa nguvu ya kila siku.


Kwa mara nyingi mama mjauzito anashauriwa aongeze uzito kati ya 25 pound mpaka 35 pounds lakini usifuatishe sana hizi namba kwani kila mtu ni tofauti. Ili mradi unakula chakula bora kwa mama mjamzito basi usiwe na wasiwasi wa kuongezeka kwani mwili wako unajua ni kiasi gani unahitaji kwa ajili yako na mtoto.

Pia ukumbuke kuwa kutokuwa na uzito wa kutosha utasababisha mtoto kuzaliwa na uzito mdogo ambayo ni chini ya 5 pounds hii inaweza kusabibisha mtoto kuzaliwa na magonjwa au kushindwa kukua vizuri au kuzaliwa njiti.

Pia ukiongezeka uzito kupita kiasi kutafanya mtoto awe na uzito mkubwa kupita kiasi kitu ambacho kitasababisha kuongezeka muda wa labour, matatizo ya kuzaa, kuzaa kwa operesheni au c-section.

Hivyo ni muhimu sana mama kubalance na kuongezeka kwa uzito unaotakiwa kwa afya yake na mtoto.
Pamoja na kula chakula bora kwa mama kumbuka kupata mazoezi maalum ya mama mjamzito ya kutosha kila siku. Hii itasaidia mwili wako kutumia virutubisho vya chakula vizuri na itasaidia pia pale utakapozaa mwili kurudi kiurahisi zaidi.

Kuhusiana na upunguaji wa uzito wa uzazi, ni kweli kila kukicha tunasikia story za watu maarufu au macelebrity ambao wamepungua sana pale wanapotoka kuzaa na hivyo wanawake wengi huwa na dhamira ya kupungua tu pale watakapozaa. Ila ni vizuri kukumbuka kuwa ulitumia miezi tisa kuongezeka mwili wako ili kujitosheleza wewe na mtoto hivyo vile vile jipe japo miezi tisa ili upungue.

Jumanne, 19 Desemba 2017


Njia 6 za kukabiliana na tatizo la kuziba kwa mirija ya uzazi


Kuziba kwa mirija ya mayai ya uzazi ni moja yaa sababu kubwa inayoweza kumpelekea mwanamke asipate ujauzito na hili ndilo chanzo kikuu cha wanawake wengi wanaoshindwa kupata ujauzito. Mirija hii ya uzazi ndimo ambamo mayai ya mwanamke hupita.

Mirija ikiziba ni kusema yai halitaweza kupita ili likutane na mbegu za mwanaume ili mimba iweze kutungwa nah ii ndiyo moja ya dalili kuu ya mirija ya uzazi kuziba. Mirija ya mayai hujulikana pia kwa kitaalamu kama ‘fallopian tubes’.

Sababu kuu ya kuziba kwa mirija ya uzazi ni maambukizi ya mara kwa mara ukeni ambayo hujipenyeza hadi ndani ya kizazi na kushambulia sehemu ya ndani ya kizazi na mirija. Maambukizi haya huambatana na muwasho, usaha ukeni, kutokwa na damu na uchafu wakati wa tendo la ndoa na kusikia maumivu chini ya kitovu.

Kuna wakati mirija haizibi bali hutokea mirija kuongezeka umbo sababu ya maji kujaa katika mirija ya maji na hivyo kupelekea mbegu za mwanaume kushindwa kupita kirahisi ili kukutana na yai. Halii hujulikana kitaalamu kama ‘hyrosalapinx’.

Dalili zitakazokuonyesha una tatizo la kuziba mirija ni pamoja na:

1. Maumivu chini ya kitovu ya mara kwa mara

2. Kusikia maumivu wakati wa tendo la ndoa

3. Kushindwa kupata ujauzito

4. Kutokwa na uchafu ukeni wenye harufu kali

Sababu ya mirija ya uzazi kuziba:

mbegu-za-maboga

>Magonjwa ya zinaa (PID)
>Upasuwaji uliopita wa sehemu ambazo si za kawaida kama katika tumbo na katika kizazi
>Mimba kutunga katika mirija ya uzazi (extopic pregnancy)
>Yai kutunga katika mdomo wa kizazi
>Utowaji mimba kila mara
>Mwili kuchafuka tu kwa ujumla

Nini unaweza kufanya ukigundulika mirija ya uzazi imeziba?

Kwanza fanya vipimo uonapo unatafuta ujauzito na hupati kwa kipindi cha walau mwaka mmoja. Kuna wengine wakiingia tu kwenye ndoa mara moja anahitaji kupata mtoto, hapana unaweza ksubiri hata mwaka ndipo ufanye vipimo. Vipimo vinapobaini ni kweli una tatizo la kuziba mirija ya uzazi unaweza kufanya yafuatayo kujinusuru na hali hiyo:

Njia 6 za kukabiliana na tatizo la kuziba kwa mirija ya uzazi

1. Acha vilevi vyote
2. Acha stress
3. Acha nyama nyekundu
4. Fanya mazoezi ya viungo kila siku
5. Kula sana matunda, mboga majani, mafuta ya zeituni, mafuta ya asili ya nazi
6. Kupata vitamin C kwa wingi tumia unga wa majani ya mlonge, kuongeza kinga yako ya mwili kwa ujumla tumia mbegu za maboga kila siku

Fuatilia mabadiliko haya kwa miezi miwili mpaka 6
TIBA YA KANSA IPO?
Tiba ya kansa ipo Ni swali ambalo kila mtu anauliza na madaktari wameshindwa kutoa majibu ya uhakika hata mimi huwa najiuliza, maana nimeshuhudia watu wengi wakipata shida juu ya tatizo hili. Madactari watakwambia una kansa ya ini, utumbo, mapafu ama kizazi, lakini hawakwambii nini kimekufikisha kwenye tatizo husika, hivo tiba ya kisasa italenga moja kwa moja katika kutibu dalili ya kansa kama kuukata uvimbe kabla haujaenea sana, kuchoma uvimbe kwa kutumia mionzi, ama kutumia madawa makali katika kudhoofisha uvimbe wa saratani. Lakini je ulishawahi kujiuliza nini chanzo kikubwa cha tatzo hili ambalo linamaliza maisha ya wapendwa wetu kila siku.??
Tiba asili ama functional medicine inahimiza kwa mgonjwa na dactari kukaa pamoja na kuchunguza nini vyanzo vya ugonjwa. Hivo kwa kusuluhisha chnazo basi tayari unakuwa umetibu matokeo ambayo ndio dalili za ugonjwa. Hivo kwa upande wa tiba asili, mwili ni kama bustani ama shamba nzuri. Shamba hili lisipotunzwa vizuri basi magugu yataanza kuota na kumea.
Tiba ya mionzi na kukata sehemu ya mwili iliyoathiriwa na saratani siyo mbaya, lakini pia ni muhimu mgonjwa kufahamu njia sahihi za kujikinga ama kuzuia tatizo lisirudi tena.

KUTUNZA SHAMBA yaani mwili wako ni sheria ya kwanza katika kukinga mwili dhidi ya saratani
Tafiti zinaonesha kwamba kuna vitu vingi ambavyo tuviweka kwenye kundi la vihatarishi vinavyoweza kupelekea sararatani, mfano aina ya lishe, ukosefu wa mazoezi, msongo wa mawazo, sumu kwenye mazingira, vyote vinaweza kuchochea ukuaji wa saratani.
Hapa utagundua kwamba ili mmea ama mifumo yako ya mwili ikiwemo viungo kama moyo, figo nk viweze klufanya kazi vizuri basin i lazima pawepo na mazingira salama kwenye shamba ama mwili husika wa binadamu, vinginevyo hapatukuwa na usawa na ndipo magonjwa kama saratani yataanza kuibuka.
Sasa kumbe tunaweza kuimarisha kinga ya mwili na kuwa makini kwenye vyakula tunavyokula, tukabadilisha mtindo wa maisha ukawa siyo wa kutegemea vyakula vya viwandani.pia tunaweza kuimarisha uwezo wa mwili kundoa sumu, na kuweka uwiano katika vichocheo ama homoni, na pia kuhakikisha tunakuwa fikra chanya mda mwingi tukaondoa msongo wa mawazo na hivo kutengenea maingira ya hisia nzuri za mwili.
Saratani ama kansa ni matokeo ya kuwa na uwiano mbaya kwenye mifumo yetu ya mwili na hivo kupelekea kinga ya mwili kushindwa kupambana na seli hizi. Seli za saratani huanza zikiwa ndogo sana lakni miili yetu iliumbwa kupambana na magonjwa , hivo ni muhimu mwili kupaliliwa na kuwekewa virutubisho vya kuusadia uendelee kupambana na seli hizi za kansa kabla hazijaleta madhara.

Ifuatao ni hatua tano ambazo unaweza kuzitumia kuzuia saratani, ama kama tayari umeugua basi itakusaidia kuzuia kuenea kwa seli za saratani ndani ya mwili.
1.ACHANA NA SUKARI
Sukari husaidia kukua haraka kwa seli za saratani, na pi kukufanya kuwa na uzito mkubwa na kitambi., kisukari kinaathiri zaidi ya watu bilioni 1.7 duniani.

Punguza matumizi ya vyakula vya wanga na sukari, pia vilivyosindikwa na badala yake tuwe tunatumia zaidi vyakula vya mafuta, asili na visivyosindikwa.
2.EPUKA VYAKULA VINAVOLETA MZIO AMA ALEJI
Viambata kama glutein vinavyopatikana kwenye nafaka za ngano kwa kiasi kikubwa, vinapoingiau kwenye utumbo hupelekea kulegea kwa ukuta wa tumbo unaohusika na uvyonzaji wa chakula, hapa nataka uelewe kwamba katika mfumo wa chakula, sehemu panapofanyika uvyonzaji wa virutubisho hitwa small intestine ama utumbo mwembamba, hivo basi siyo kila kitu huruusiwa kupita hapa kwenda kwenye mfumo wa damu. Sasa kuta za utumbo ni kama chekecheke ambalo linazuia baadhi ya vitu hatari kupita kwenda kwenye damu, endapo chekecheke hili likiwa na matobo makubwa ndipo sumu na protin kubwa kama glution hupenya kuelekea kwenye damu. Na hapo mwili utaitikia kama adui kaingia hivo kupeleka askari wengi mahali husika kushambulia, sasa mashambulizi ya mara kwa mara hupelekea mahali husika kututumka na kuvimba.
3.IMARISHA MFUMO WAKO WA CHAKULA
Saratani nyingi hutokana na hitilafu kwenye mfumo wa chakula unaoteketezwa na lishe mbaya, hakikisha unapunguza kiasi cha protini kwenye mlo wako, badala yake tumia vyakula salama vya mafuta kama mayai ya kuku wa kienyeji, nyama kutoka kwa mnyama aliyekuzwa kwa kula majani na siyo nafaka, parachichi, na nazi. Tumia pia mafuta ya omega 3 kwa wingi kutoka kwenye vyanzo kama samaki ama unaweza kupata virutubisho hivi vya asili kutoka kwenye vyanzo sahihi.
4.MAZOEZI IWE NI KITU CHA LAZIMA
Kwa ujumla mazoezi hupunguza kasi ya utolewaji wa homoni ya insulin na hivyo kutengeneza mazingira hafifu ya uwepo wa sukari kwenye mwili, na hivo sukari ikiwepo kidogo hupunguza kasi ya kuenena kwa seli a kansa. Utafiti ulowahi kufanyika umeonesha kwamba mazoezi mfululizzo kwa miezi mitatu yanasaidia kuimarisha kinga ya mwili inayopambana na seli za kansa/saratani.
5.PATA USINGIZI WA KUTOSHA NA KUJIEPUSHA NA mazingira hatarishi yanayopelekea kuugua ugonjwa wa saratani, mazingira haya ni kama mionzi kutoka kwenye vifaambalimbali kama matumizi makubwa ya simu, tv, kemikali zinazotokana na dawa za kuua vimelea kwenye mimea na wanyama.
UTAFITI WA MIMEA UNASEMAJE KUHUSU TATIZO LA KANSA
Nchi kama china na Vietnam zinasifika kwa kuzalisha kwa wingi mimea mbalimbali ambayo imekuwa ikisaidia kutibu kansa stage ya kwanza na kusaidia kuzuia kusambaa kwa seli za kansa. Hivo gharama zake imekuwa kubwa sana ukizingatia mimea hii haipatikani hapa Africa. mimea hii ni kama
1. GINSENG, mmea huu husaidia
· kuongeza kiwango cha seli nyeupe za damu ambazo hupambana na seli a kansa, rejea hapo juu nlipoandika uhusiano wa kinga yako na kukua kwa seli za saratani.
· Pia mmea huu husaidia kharakisha uponaji wa vidonda na kutibu saratani ya awali.
2. CORDCEP SYNESIS husaidia
· Kuimarisha kinga ya mwili na hivo kuzuia mashambulizi ya mwili ya mara kwa mara
· Kupambana na seli za kansa
· Huimarisha ufanyaji kazi wa figo, ini na mapafu na
· Kuongeza nguvu kwa wale wanaopata ganzi mara kwa mara.
3. GARNODERMA, mmea huu husaidia
· kuimarisha kinga ya mwili na hivo kuzuia saratani.
· Kupunguza athari zinazotokana na tiba ya mionzi na madawa makali (radiotherapy na chemotherapy) nahivo kukupunguzia adha mablimbali kama kutapika, maumivu, kupungua kwa nywele, na ganzi ya mara kwa mara. Hivo unaweza kuendelea na dozi ya hospitali huku ukitumia dawa zetu pia.
· Kuongeza uwezo wa kinga ya mwili, na kusaidia wenye aleji na magonjwa ya mfumo wa hewa kama pumu na hivo kukuwezesha kurahisisha upumuaji.

Jumatatu, 18 Desemba 2017

FANGASI SUGU SEHEMU ZA SIRI NA NAMNA YA KUKABILIANA NAYO;
Idadi kubwa ya watu wanasumbuliwa na tatizo la kuwashwa sehemu za siri bila kujali jinsia na umri.Tatizo hili laweza kusababishwa na matatizo mbalimbali lakini kubwa ni fangasi.
Watu wanapaswa kufahamu kuwashwa sehemu za siri kunaweza kuwa dalili ya maradhi fulani ndani ya mwili kama vile mzio,matatizo ya ngozi au sumu ya mimea au wadudu ambao wanakawaida hiyo.
Mara nyingi muwasho sehemu za siri unaosababishwa na kitu huisha wenyewe au muda mfupi baada ya kitu hicho kikiondolewa.Kuondolewa kwa kitu hicho kunakuwa ni matibabu sahihi na kuendelea na njia bora za kujikinga kutopata maambukizi tena.
Vitu vingine vinavyosababisha muwasho huhitaji matibabu.
Ikiwa unawashwa kwa muda mrefu ni vyema kuzungumza na daktari.Kukaa na ugonjwa kwa muda mrefu kunaweza sababisha ugonjwa kusambaa mwilini na kuongeza hatari ya kifo.

KISABABISHI;
Kuwashwa uume au sehemu zingine za siri za mwanaume husababishwa na sababu zilezile zinazosababisha muwasho sehemu zingine za mwili.Maradhi ya fangasi husababisha muwasho kwa wanaume wengi ,sababu zingine ni kama ugonjwa wa upele,kuwepo kwa chawa,mzio na maambukizi mengine ya bakteria.Maambukizi hasa ya magonjwa ya zinaa ndio chanzo cha kuwashwa uume.

FANGASI SEHEMU ZA SIRI;
Maradhi ya fangasi(Candidiasis)husababishwa na vimelea viitwavyo Candida albicans.Vimelea hivi hushambulia jinsia zote ingawa hushambulia zaidi jinsia ya kike kutokana na maumbile yao na hali ya kuwa na unyevunyevu mara nyingi.Mazingira hayo husababisha fangasi kumea vizuri.Watu wengi wana vimelea hivi katika miili yao kwa kiwango kidogo.Kinga ya mwili ikisaidiwa na bakteria walinzi wa mwili huweza kupambana na vimelea hivi.
Mtu anapokunywa dawa za kuua bakteria kutokana na ugonjwa mwingine wa bakteria kama kuhara damu,husababisha bakteria walinzi wa mwili kufa hivyo kuongeza hatari ya mwili kushambuliwa na ugonjwa wa fangasi.Ikiwa kinga ya mwili itashuka kutokana na maradhi kama VVU au lishe duni mwili utakuwa katika hatari zaidi ya kupata maradhi ya fangasi.
Hata hivyo maradhi ya fangasi yanaweza kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kwa kuchangia nguo au vifaa vya kuogea na kujamiiana na mwathirika.Wanaume wengi wanasumbukiwa na fangasi sehemu za siri huishi maeneo yenye joto sana kama pwani,lindi,Mtwara,Tanga na Dar es Salaam.
Kuishi sehemu yenye joto pamoja na kuvaa nguo za kubana hasa zisizotengenezwa na pamba kwa asilimia 100kunafanya sehemu za siri kuwa na unyevunyevu hivyo kutengeneza mazingira mazuri kwa fangasi kuzaliana na kuongezeka.

DALILI ZA FANGASI SEHEMU ZA SIRI;
Sehemu za siri mara nyingi hutumiwa kama maficho ya fangasi.Hizi ni kama vile uume,korodani,katika mapaja,uke,na sehemu za katikati ya makalio.Wakati mwingine fangasi husambaa hadi kwenye mapaja.Kwa wanaume fangasi huweza kusababisha sehemu za siri za mwanaume kubadilika na kuwa nyekundu na hata kuwasha.
Ngozi inayozunguka sehemu hizo huwasha ,kukakamaa na kutoa majimaji ambayo hutoa harufu mbaya.

MATIBABU YA FANGASI;
Ikiwa una dalili za ugonjwa wa fangasi ni vyema kufika kwa daktari kwa ajili ya matibabu na ushauri zaidi.Kutumia dawa bila ushauri wa daktari kunaweza kusababisha kutopona kabisa ,kutopona vizuri au ugonjwa kujirudia baada ya siku chache.Vimelea pia vinaweza kujenga usugu wa dawa.
Kumwona daktari kutasaidia kujua kama una maradhi mengine yanayosababisha upate fangasi sehemu za siri.Ugonjwa wa fangasi usipotibiwa husambaa kwenye damu na kusababisha madhara makubwa mwilini kama kwenye ubongo na mapafu.
JINSI YA KUJIKINGA;
Ili kusaidia kuepuka kupatwa na fangasi sehemu za siri ni vyema kuosha vizuri.Kwa wale wanaume ambao hawajatahiriwa wanapaswa kuosha kwa umakini zaidi hadi sehemu za ndani a govi.kwa kifupi ni vizuri sehemu za siri kubaki wakati wote katika hali ya usafi na ukavu,kwa maana ya kutokuwa na unyevunyevu unaweza kusababisha maambukizi.
Matumizi ya poda maalum yanaruhusiwa hasa kipindi cha joto kali ili kuzuia unyevunyevu.Vaa nguo isiyobana ,iliyotengenezwa kwa vitu asilia kama pamba.Badili nguo ya ndani angalau kila siku na tumia kinga pale unapokutana kimwili na mtu ambaye hujui hali yake kiafya.