Ijumaa, 29 Desemba 2017

MATATIZO YA KUKOSA HEDHI KWA WANAWAKE
Wanawake wengi huwa na vipindi vya hedhi kuanzia 11 mpaka 13 kwa mwaka. Hii hutofautiana kwa wanawake. Unaweza kuwa na vipindi zaidi ya hivi au vichache. Kukosa hedhi au kubadilika kwa vipindi vya hedhi itatazamwa kutokana na kile ambacho ni kawaida kwako. Mfano ikiwa unakuja kwenye hedhi tarehe 11-13 kila mwezi, hiyo ndiyo kawaida yako. Mwingine anaweza kuwa anakuja kwenye hedhi tarehe 20-23 kila mwezi , na hiyo ndiyo kawaida yake. Hivyo kawaida  yako inaweza ikawa si kawaida kwa mwanamke mwingine. Ni vyema kutazama siku zako na siyo za mwingine, kuangalia kama una tatizo ama la.
Vipindi vya hedhi huwa vinatofautiana sana hasa  kuelekea miaka ya kukoma hedhi. Wanawake wengi hutambua kwamba wanaelekea karibu na kukoma hedhi  pale vipindi vyao vya hedhi huanza kubadilikabadilika na kutokuwa vya kawaida. Kukoma hedhi hutokea pale unapokuwa na  kipindi cha mwaka mzima (miezi 12) bila kupata hedhi au kwa maneno mengine  miezi 12 tokea umepata hedhi yako ya mwisho.

                                       
Mara nyingi ujauzito ni sababu ya kukosa hedhi. Kama unadhani wewe ni mjamzito tafadhali anza kuishi kama mwanamke mjamzito mpaka pale ukapogundua ya kwamba kweli wewe ni mjamzito ama la. Tumia vipimo vya ujazito vinavyopatika kwenye maduka ya dawa kujipima. Ni rahisi kutumia. Unaweza kusoma maelekezo au kuelekezwa na muuzaji.

SABABU ZA KUKOSA HEDHI AU KUWA NA HEDHI ISIYO YA KAWAIDA

Nimesema sababu ya kwanza kabisa ya kukosa hedhi ni ujauzito. Kama umekosa hedhi na huna kabisa ujauzito, vipo visababishi vingine kama ifuatayo:
  Kuongezeka sana au kupungua sana  uzito wa mwili. Ingawa mara nyingi kupungua uzito ndilo tatizo la mara kwa mara kumfanya mwanamke kukosa hedhi au kuwa na hedhi isiyo ya kawaida lakini pia kuongezeka uzito kunaweza kusababisha matatizo ya hedhi.
 Matatizo ya ulaji mfano kukosa hamu ya kula au matatizo yajulikanayo kwa kitaalam kama  bulimia na  anorexia nervosa.  ‘Bulimia’ ni tatizo ambalo mtu hula sana lakini mara tu baada kula hutapika chakula chote na kufanya mtu huyo kukonda sana na ‘Anorexia nervosa’ ni tatizo ambalo mtu hukosa hamu ya chakula na kumfanya ale chakula kidogo kisichokidhi mahitaji ya mwili .  Hii inampelekea kupoteza uzito
    Kufanya mazoezi ya viungo sana
    Msongo wa mawazo
 Kuumwa
Safari
Madawa kama dawa za uzazi wa mpango. Hizi zinaweza kukufanya ukawa na hedhi nyepesi, isiyo ya mara kwa mara au  kuwa na hedhi mara kwa mara au kuruka vipindi vya hedhi au kukosa hedhi kabisa
   Matatizo ya homoni. Matatizo ya homoni yanaweza kubadili kiwango cha homoni ambacho mwili huhitaji kwa ajili hedhi
   Matumizi mabaya ya madawa
  Matatizo kwenye viungo vya kiunoni kama uvimbe kwenye mji wa mayai ( Polycystic Ovary syndrome, kuziba kwa kiwambo cha uke ( imperforate hymeni) na uvimbe wa kovu kwenye kuta mfuko wa uzazi (  Asherman’s syndrome)
 Kunyonyesha. Wanawake wengi hawezi kurudi kwenye siku zao za kawaida mpaka wanapoacha kunyonyesha

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Comment yako ni muhimu sana